Unapozungumzia Kiwanda cha Bongo Movie, lazima utatazama wasanii walioitoa Bongo Movie iliko kuwa hadi hapa ilipo au ilipofia. Wasanii hawa wanaweza wakawa mifano kwa wengine iwe kwa uzuri au ubaya, zamani wasanii wa Bongo Flava (wa kiume) walikuwa wanafanya juu chini wawe wakubwa kimuziki watoke na wasanii wa Bongo Movie, Filamu ilikuwa juu zaidi ya Bongo Flava hasa kwenye upande wa umaarufu wa wasanii, imagine enzi hizo kuna tetesi za mtu kuwa kwenye mahusiano na Wema Sepetu au Wolper au Uwoya au Johari au Batuli au Kajala au Aunty au Jokate n.k, Magazeti ya udaku walikuwa wao kwa kiasi kikubwa, umaarufu ukawa mkubwa kuliko kipato chao.
Siasa ikaingia kati sababu ya nguvu yao kwenye jamii, ikawasomba na wakazamia huko, wengine hadi leo ni machawa wa serikali wakisahu kabisa kazi zao. Bongo Flava waliwahi jaribu hili, ila kupotea Kwa Marlaw baada ya Kampeni za mwaka 2010, kila msanii akawa anaogopa kutumbukia mazima kwa wanasiasa akiogopa kugawa watu na ikawa mbaya kwenye kazi yake. Hili liliwakomaza na kujitengenezea thamani zao wenyewe, wakati Bongo Flava wanakatiwa mpunga kwenye kampeni zilizo fwata, Bongo Movie wao wanapandishwa Costa kupiga makofi tu na hela ya maji.
Tukirejea kwenye kauli ya Baba Levo, Kila mmoja amereact kivyake kuhusiana na kauli hii kuwa Bongo Movie ni Kama nyumbu sababu ya kutojitambua. Lakini Wengi wao ni hawa walio chipukia kwenye tamthilia za hivi karibuni, wamekuwa mavixen wakajikuta kwenye uigizaji. Filamu ni kazi rasmi, sio ya kutafutia umaarufu au plan B, kuna watu wameifanyia makubwa tasnia ya filamu ila maisha yao hayaendani na kile walicho kifanya, hasa hawa ndio walioitwa Nyumbu sababu wengi wao wameamua kuwa rahisi zaidi kwenye maisha yao, hawajataka kugeuza uchungu wa kufanya kazi zao kwenye mazingira magumu enzi hizo kuwa fursa ya kupata kikubwa nyakati hizi.
Hawapaswi kukasirika kuitwa Nyumbu, wanapaswa kuangalia wanakosea Wapi na kujifunza
#Sojamedia