Bosi Mpya Simba Kujulikana Januari 29, 2023 Waeleza Sifa Za Wagombea…


KAMATI ya Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Simba, umeweka wazi kwamba, Januari 29, 2023, itakuwa ni siku rasmi ya wanachama wa klabu hiyo kuchagua viongozi wapya.


Kwa sasa, Murtanza Mangungu ambaye ni Mwenyekiti wa Simba, anakwenda kumaliza muda wake, huku kwa mujibu wa kamati hiyo, anaruhusiwa kugombea kwa mara nyingine.


Akizungumza na Spoti Xtra, Boniface Lihamwike, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Simba, alisema kwa hali ilivyo, viongozi waliopo madarakani wanaendelea kuongoza klabu hiyo kwa mujibu wa katiba.



Mjumbe wa kamati ya uchaguzi Simba, Dkt. Gerald Mongela.

“Sifa za viongozi zinafahamika na miongoni mwao katika kanuni ya 6 ya Uchaguzi Simba inaeleza lazima awe mwadilifu na kiwango cha juu cha uaminifu, mwanachama hai wa Simba, shahada ya chuo kikuu (Mwenyekiti), Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi lazima awe na elimu ya kidato cha nne, uzoefu uliothibitika miaka mitatu, asiwe amepatikana na hatia ya kupewa adhabu ya kufungwa na awe na angalau miaka 25 hadi 60, asiwe mwanahisa au mwamuzi wa mpira wa miguu.


“Nafasi ambazo zinagombewa ni Mwenyekiti nafasi moja, Mjumbe mmoja awe na shahada na wajumbe wanne elimu kidato cha nne. Mwenyekiti atakapochaguliwa atateua wajumbe wawili katika nafasi za wajumbe wanne mmoja angalau awe mwanamke.


“Desemba 5 hadi 19, 2022 ni kuchukua fomu ofisi za Simba, Desemba 20 na 21 ukaguzi za fomu za wagombea. Desemba 22 na 24 usaili wa watia nia waliorudisha fomu kwa muda.


“Desemba 28 kubandika majina ya wagombea waliopita, Desemba 29 na 30 kupokea mapingamiza, Januari Mosi hadi 2, 2023 kupitia mapingamiza, Januari 3 na 4 kusikiliza mapingamiza.


“Januari 5 kutangaza majina ya wagombea waliokidhi vigezo, Janauri 6 hadi 28 kampeni na Januari 29, 2023, utafanyika uchaguzi na kusomwa matokeo yake,” alisema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad