Brazil iliungana na Ufaransa katika hatua ya mwondoano kwenye Kombe la Dunia siku ya Jumatatu, Novemba 28, baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Switzerland.
Portugal.
Cristiano Ronaldo (kushoto) na Bruno Fernandes wakishangilia baada ya kushinda mechi ya Kundi H dhidi ya Uruguay. Picha: Odd Andersen. Chanzo: Getty Images
Kiungo wa kati wa Brazil, Casemiro ndiye alifunga bao la kipekee ambalo liliwasadia washindi hao mara tano wa Kombe la Dunia kufuzu katika Kundi G.
Huku Brazil hao wakikosa huduma za nahodha wao nyota Neymar aliyejeruhiwa, walionekana kana kwamba wangekuwa na ulazima wa kusawazisha kwa pointi moja baada ya bao la Vinicius Junior katika kipindi cha pili kukataliwa kwa msingi wa kuotea.
Lakini zikiwa zimesalia dakika saba kwa mechi hiyo kutamatika, Casemiro ambaye huchezea Manchester United, alichonga ndizi hadi kimyani akimchenga Manuel Akanji na kuvunja ngome ya Mswizi huyo mahiri.
Kikosi cha Tite ni timu ya pili kufuzu kwa hatua ya 16 bora baada ya Ufaransa na pia ni timu pekee mbali na watetezi kushinda mechi zote mbili za makundi nchini Qatar.
Brazil walianza kampeni yao nchini Qatar kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Serbia lakini walipata pigo baada ya fowadi wa Paris Saint-Germain Neymar kupata jeraha la kifundo cha mguu.
Ronaldo
Wakati huo huo kiungo wa Manchester United Bruno Fernandes alifunga bao lake la kwanza katika Kombe la Dunia na kusaidia Ureno kufuzu kwa duru ya 16.
Fernandes alifungia Ureno mabao mawili katika mechi dhidi ya Uruguay wakati wa pambano la pili la Kundi H lililosakatwa kwenye Uwanja wa Lusail.