Cheed "Music Labels Hazina Faida BORA Kuwa Peke Yako

 


Kuna Interview ya Cheed nimeisikiliza mpaka nikacheka. Jamaa anasema kwamba Lebo hazina faida na wasanii waliopo Nje ya Lebo ndio wanafanya Vizuri zaidi, akataja Mfano Dayoo, Platform, N.K.


Nimeshangaa sana kusikia kauli hii, Hivi ni Dunia gani ambayo Msanii hataki kuingia kwenye Lebo? Cheed anadhani kwamba Dayoo na Platform hawataki Lebo? Pia ni aibu kubwa kwa mkongwe kama Cheed Kumtumia Dayoo na Platform kama mfano wa watu waliofanikiwa kwenye muziki.


Leo Hii Harmonize, Rayvanny, Zuchu na Mbosso wapo hapo kwa sababu ya WCB. Asake, Ayra, Tems, Ruger, Fire boy wanatisha kwa sababu wapo kwenye lebo.


Lebo zingekuwa hazina faida leo hii Sony, Warner, Universal, Atlantic, Def Jam zingekuwepo kutafuta nini? Wasanii si wangezikimbia. Sasa huyu Cheed anapata wapi kiburi cha kusema ukiwa nje ya Lebo ndio unatoboa kimuziki?


Hivi kufeli kwake King's Music na Konde Gang ndio kunampa Conclusion kwamba Lebo ni mbaya? Cheed na Mwenzake wajiongeze, wana talent ila wanaimba nyimbo ambazo kwa sasa hazina mashabiki, IMBENI NYIMBO ZA KUCHEZEKA, SIO KILA NYIMBO KULIA LIA TU.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad