Club Africain wafanyiwa vurugu Uwanja wa Mkapa




Klabu ya Young Africans huenda ikakumbana na adhabu kutoka Shirikisho la soka Barani Afrika CAF, kufuatia vitendo visivyo vya kiungwana walivyofanyiwa baadhi ya maafisa wa Club Africain ya Tunisia.

Vitendo hivyo vimetokea kabla ya kuanza kwa mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa leo Jumatano (Novemba 02), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kwa kuthibitisha ushahidi kwa njia ya Video, Club Africain imeweka Video ya vitendo walivyofanyiwa maafisa wake wakati wakiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, inayoonyesha maafisa hao wakimwagiwa maji na Makomandoo wa Young Africans na kuzuiliwa kuingia katika moja ya vyumba vya Uwanja huo.

Video hiyo iliyowekwa katika ukurasa wa Facebook wa Club Africain ilikua ikirushwa Mubashara, kwa makusudi ya kuuonyesha umma yale yaliyotokea Uwanja hapo dakika kadhaa kabla ya mchezo huo kuanza.

Mbali na kuweka video hiyo, Club Africain imerikodi matukio yote waliyokutana nayo kabla na baada ya kufika Uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa ni pamoja na changamoto ya Foleni iliyokuwepo katika eneo la Uhasibu wakati wakielekea Uwanjani hapo.

Hata hivyo CAF ndio wenye maamuzi ya mwisho endapo Club Africain watawasilisha malalamiko ya kufanyiwa vitendo hivyo walipokua Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuyatolea maamuzi kwa mujibu wa Ripoti ya Msimamizi mkuu wa mchezo huo wa Mkondo wa Kwanza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad