Dar, Mwanza Zaongoza kwa idadi ya Watu Nchini

 


Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaam limetajwa kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu nchini kwa kubeba asilimia 8.7 ya Watanzania wote huku jiji la Mwanza likifuatia kwa kuwa na asilimia 6.


Dar es Salaam hadi sasa kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 una wakaazi zaidi ya milioni 5.38.


Hayo yamesemwa leo Oktoba 31 na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akitangaza matokeo ya awali ya Sensa ya watu na makazi jijini Dodoma.


Amesema idadi hiyo ya watu imefanya kuwapo kwa malalamiko mengi ikiwa kuna upungufu wa huduma yoyote.


 "Malalamiko huwa yanakuwa mengi kwa sababu watu wengi wako pale," amesema Samia.


Mkoa unaofuata kwa kuwa na idadi kubwa ya watu nchini ni Mwanza ulio na wakazi zaidi ya milioni 3.69 milioni ikiwa ni sawa na asilimia 6 ya Watanzania.


"Kwa Tanzania Zanzibar, mkoa wenye idadi zaidi ya watu ni Mjini Magharibi wenye jumla ya watu 893,169 sawa na asilimia 47.3 ya wakazi wote wa Zanzibar.


"Hii ina maana kuwa mkoa huu una watu wengi zaidi, watu wamekusanyana hapo zaidi," amesema.


Mkoa wa Kaskazini pemba unafuata kwa kuwa na watu 272,091 sawa na asilimia 14.4 ya watu wote wa Zanzibar

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad