Diamond Platnumz "Tuache Kushindana Wenyewe kwa Wenyewe, Tushindane na Wanigeria"


Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare ameahidi kukutana na Ziiki na Spotify kujipanga namna ya kupambana na #Uharamia wa kazi za Muziki katika mitandao hiyo.

Doreen ameyasema hayo katika Leo Novemba 23,2022 katika Kongamano la Wasanii wa Muziki la Masterclass iliyoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, COSOTA na Ziiki Media iliyofanyika Jijini Dar es Salaam ya kuwajengea uwezo wasanii namna ya kupeleka kazi zao katika mtandao Kimataifa.

Akizungumza katika Kongamano hilo Mbunge wa Morogoro Hamis Taletale na Meneja wa Msanii Nasibu Abdul maarufu kama @diamondplatnumz ameiomba Ofisi ya Hakimiliki Tanzania kuzungumza na Spotify kuona namna bora wanaweza kuthibiti uharamia wa kazi za Muziki katika digital platforms ikiwemo Spotify.

"Ombi letu kwa COSOTA nikusaidia fedha zinazopatikana katika Mtandao wa Spotify ambazo hazimilikiwi na wahusika na baada ya kubainika watu hao siyo wamiliki Mapato yake yawe yanapelekwa COSOTA ili kuwafiikishia wasanii husika,"alisema Mhe.Taletale.

Pamoja na hayo nae Msanii @diamondplatnumz ametoa ushuhuda wa safari yake ya Muziki na namna ambavyo ameweza kufanikwa kuvuka mipaka na kuupeleka Muziki wa Tanzania Kimataifa katika Kongamano hilo na kusema aliweka mkakati ya kuanza kushika mashabiki Afrika Mashariki na baadae Afrika na pia kutumia njia ya mtandao kusambaza kazi zake.

"Kazi ya kuweza kuupeleka Muziki Kimataifa ni suala la kimkakati lazima kuwa na mpango ambao utaandaa kazi ambazo kulingana na beats zake na mashairi yatavutia hata mataifa ya nje," alisema Diamondplatnumz.

Pamoja na hayo nae Msanii huyo alitoa msisitizo Kwa wasanii kuweza kutambua mtandao ambao unafanya vizuri na kutoa malipo yenye fedha nyingi katika usambazaji wa kazi za Muziki ambapo alieleza kuwa amefanikiwa kupata fedha nyingi kupitia mtandao wa Spotify.

Aidha, Msanii Diamond Platnumz alisisitiza suala la mashabiki kuacha kuwachonganisha na kuwapambanisha na wasanii wengine bila kuelewa suala la Muziki linahitaji umoja ili kuweka kuikuza tasnia na kufikia soko la kimataifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad