DOGO JANJA @dogojanjatz au Janjaro; ni staa mkubwa wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye aliingia kwenye sanaa kwa namna ya ajabu kabisa. Licha ya Arusha anakotoka kuwa na historia ya kutoa wanamuziki wengi, wazuri wa kitaifa na kimataifa, lakini aliibuliwa na kijana kutoka Manzese jijini Dar, Madee.
Katika maisha yao ya kupendana na Uwoya @ireneuwoya8 , Dogo Janja alifunga ndoa yenye utata na mwanamama huyo hivyo wengi kuona kama ilikuwa ni maigizo; Katika mahojiano maalum (exclusive) na mwandishi wetu, Dogo Janja anafunguka mengi kama ifuatavyo;
IJUMAA SHOWBIZ: Hebu tueleze ukweli kuhusu ndoa yako na Uwoya, ilikuwa ndoa ya kweli au maigizo?
DOGO JANJA: Ile ilikuwa ndoa ya kweli na nikiri tu kwamba hatukuwashirikisha wazazi.
IJUMAA SHOWBIZ: Kwa nini kitu kikubwa kama hicho msishirikishe wazazi?
DOGO JANJA: Kwa kweli tulifanya makosa, lakini kifupi tu mimi nasema mapenzi ni upofu, naukubali usemi huo.
IJUMAA SHOWBIZ: Je, au ni kama watu wanavyosema kwamba ulilogwa?
DOGO JANJA: Kwa kweli sisi kama mastaa hatuamini uchawi; ni mapenzi tu yalitufunika usoni.
IJUMAA SHOWBIZ: Wewe ullelewa kimuziki na msanii maarufu Madee, je, naye hukumshirikisha katika hili la ndoa na Uwoya?
DOGO JANJA: Kwa kweli sikumshirikisha na yeye alidhani ni muvi, alijua ni muvi.
IJUMAA SHOWBIZ: Je, mliachana baada ya kugombana? Na je, mligombea nini?
DOGO JANJA: Hapana; hatukugombana, tulikubaliana tu kwamba hii miaka mitano inatosha, hatukuachana vibaya. Hutakiwi kuachana vibaya na x-wako; hujui nani atakuokota siku moja ukianguka.
IJUMAA SHOWBIZ: Unawashauri nini vijana kuhusu kuwa na wapenzi na kupendana?
DOGO JANJA: Nasema tu kwamba kiukweli mapenzi ya vijana hayadumu kwa sababu wanabanana sana na wengine inatokea mpenzi wako hakuheshimu ipasavyo hivyo pendo linakwisha ghafla.
IJUMAA SHOWBIZ: Nini kinatakiwa kwa vijana ili penzi lao liweze kudumu?
DOGO JANJA: Njia ni moja tu; ni kwamba inatakiwa uaminifu kwa sababu hata mgombane vipi kama ni mkeo mtalala kitanda kimoja na kujifunika shuka moja.
IJUMAA SHOWBIZ: Ikitokea mwanamke ndiye mgomvi na siyo wewe mwanaume, unawashuri wafanye nini vijana wanaokumbwa na hilo?