Napelekeshwa zaidi na matumizi ya common sense kuliko kanuni au sheria. Kwa mfano ile sheria ya PF3...kwamba unakaribia kufa lakini manesi na madokta wanasema hawakutibu hauna PF3 kutoka Polisi...
Na tukirudi katika common sense kanuni inayomlazimisha mchezaji kumpa mwenzake mkono. Aishi Manula anamuona Prince Dube anapakaa mafuta ya Nguruwe kabla ya mechi, atampa mkono? Na mgeni wa heshima ambaye jana kanitukana Baa kwanini nimpe mkono? Ndio maana Wazungu wakaamua fair play isiwe lazima. Zaha hapigi magoti wakati issue hizi za kupiga magoti kabla ya mechi haijaanza.
Hakuna adhabu. Ferdinanes waligoma kumpa mkono John Terry. Hakuna adhabu. Suarez aligoma kumpa mkono Evra. Hakuna adhabu. Adhabu aliyopewa ilihusiana na masuala ya ubaguzi. Inanichekesha watu wanapodeal na kanuni ambazo zilitungwa huku nusu ya Wajumbe wakivuta sigara nje. Na waliozikubali walikuwa busy wakisubiri posho zao. Katika soka la wanawake zipo? Kuna dada zetu wa Kiislamu wamefundishwa kutompa mkono mwanaume.
Ni kama yule Mama aliyekwepa kumpa mkono Uhuru Kenyatta.......Napenda kutumia common sense kuliko kanuni kwa sababu kanuni nyingi zinatungwa na watu wasiotumia common sense, hata huku dunia ya tatu....
(Morrison na Metacha wamepiga watu wamefungiwa mechi tatu...hawa hawajasalimia wamepigwa mechi tatu, is it right?)