GSM Wampa Kijana Majaliwa Shilingi Milioni Tano



Katika kuunga Mkono juhudi za Serikali na Rais Samia Suluhu kwa kumpatia ajira kijana Shujaa Majaliwa, GSM FOUNDATION @gsmfoundationtz imeahidi kumpa Kijana huyo shilingi milioni tano ikiwa pia ni kama shukrani kwake kwa kujitoa kwa nguvu zote kuokoa Watu kwenye ajali ya Precision Air, Bukoba.

Msemaji wa GSM FOUNDATION amesema “Mwenyekiti wetu wa Taasisi hii inayojishughulisha na mambo ya kijamii Ghalib Said Mohammed (GSM) alinipigia simu jana jioni kunielekeza nitangaze support yetu Kwa kijana Majaliwa, tunajua sio jambo kubwa tulilofanya lakini tunaona ipo haja ya kumfariji Mtu huyu ambapo Yanga pia watatangaza zawadi ya kumpa Pikipiki hivi punde”

“Mbali na Shukran hizo Mimi na familia yangu pamoja na kuomba Mungu kwetu tutampatia The Heroe Majaliwa shilingi milioni moja, binafsi amenifanya nione bado tunao Watanzania ambao wapo tayari kuweka rehani roho zao kwa ajili ya kuokoa Binadamu wengine vilevile ameokoa mamilioni ya pesa ambazo bila shaka Makampuni ya BIMA yangewajibika kulipa iwapo umauti ungewafikia Watanzania wenzetu, kiukweli anastahili kutuzwa”

“Nichukue fursa hii kutoa wito kwa Taasisi na Watu binafsi wampe moyo zaidi kijana Majaliwa kwa kumpa walau mkono wa pongezi, hii itakuwa chachu kubwa ya kutengeneza Mashujaa wengi zaidi mfano wa Bwana mdogo huyo” ——— amemalizia Msemaji wa GSM Foundation

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad