Hamis Kigwangalla Amtaka Bashiru Ajivue Ubunge wa Kuteuliwa


Mbunge wa Nzega Vijijini, Dr. Hamis Kigwangalla @hamisi_kigwangalla amemtaka Mbunge wa kuteuliwa Dr. Bashiru Ally ajiuzulu nafasi ya Ubunge na aombe radhi kwa kauli zake alizoiita ni za uchochezi na zinazolenga kuichafua Serikali na Rais Samia “Huwezi kumbomoa Mwenyekiti wetu (Rais Samia) na tukakuacha, ndio maana tunashughulika nae”

“Mtu ambaye amekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, amepewa Ubalozi vyote hivi unateuliwa kwa raha, furaha na uamuzi wa Rais , sio kwamba una sifa, hata alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Mimi nilikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, sikuona cv ambayo ilimfanya apewe Ukatibu Mkuu wa Chama, anasemwa aliwahi kuwa CUF hajawahi kukanusha hatujui kadi ya CCM aliichukua lini au kadi ya CUF alirudisha lini?, anaenda kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama kinachotawala Nchi, tulishangaa lakini tuliheshimu Mamlaka ya aliyemteua ambaye alikuwa Rais, kwahiyo Dr. Bashiru atulie aheshimu Mamlaka zilizomteua, hana uzoefu kwenye Serikali wala Siasa”

“Nimeona leo nimfunde Dr. Bashiru sijui Rais wetu wa wakati ule Dr. Magufuli alimtoa wapi?, tunashangaa kumwona Dkt.Bashiru akikasirika sisi kumsifia Rais wakati anafanya mambo mazuri wakati yeye ndiye aliyetufundisha kumsifia Rais akifanya mazuri, Rais wa sasa hivi anafanya vizuri lazima tumsemee yeye anashangaa nini tukimsifia Rais kwamba anaupiga mwingi?, sasa kama yeye anaumia wakati huu ni bora akae kimya tu na sio kutoka hadharani kuongea maneno ya uchochezi "

“Dkt.Bashiru hana Jimbo alipaswa kuwa Chawa namba moja wa Rais maana kateuliwa na Rais , Jimbo lake ni Ikulu, hata kama amejipanga kuachana na siasa 2025 asiichafue Serikali, kama Ndugu Bashiru ana uungwana kidogo, ajitathimini, aombe radhi kwa Watanzania pia arudishe nafasi ya Ubunge kwa Mamlaka iliyomteua, aombe radhi na kisha aandike barua ya kuachia nafasi ya ubunge, akaendelee na harakati ili tujue sio mwenzetu kama tunampiga tujue tunampiga adui”

Itakumbukwa hivi karibuni akiwa Morogoro Dkt.Bashiru Ally alisema anakerwa na lugha za Wananchi kuwasifia Viongozi wao hata kwa mambo ambayo ni wajibu wa Viongozi kwa Wananchi “Hizi lugha za eti anaupiga mwingi, sijuieti tunakushukuru kuleta fedha sio sahihi"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad