Hawa Hapa Ndio Watu Tisa Waliokamatwa na Madawa ya Kulevya Akiwemo Kocha Simba


Watuhumiwa tisa akiwemo Kocha wa Makipa wa Klabu ya Soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam Muharami Said Sultan wanashikiliwa na Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya kilo 34 aina ya heroin.

Akizungumza leo Jijini Dar Es Salaam Novemba 15, 2022 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya amesema Mamlaka hiyo imekuwa ikifanya operesheni maeneo mbalimbali nchini kuanzia Oktoba hadi Novemba mwaka huu na kufanikiwa kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Akifafanua zaidi Kamishina Jenerala Kusaya amewataja wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo ni Kocha wa Makipa wa Simba Muharam Said Sultani(40) mkazi wa Kigamboni na kufafanua kwamba Muharam amewahi pia kuichezea timu ya Simba.

Wengine ni Mfanyabiashara na Mmiliki wa Kituo cha Soka cha Cambiasso Sports Academy kilichopo Tuangoma wilayani Kigamboni Alhaj Kambi Zeber Seif maarufu kwa jina la Kambiasso au Alhaj Kambi mbali ya kumiliki kituo hicho cha soka ana miliki kampuni ya Safia Group of Companies inayomiliki magari ya kusafirisha abiria (daladala) kutoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Pwani.

Pia Mamlaka hiyo inamshikilia Said Abeid Matwiko ambaye anaishi Magole A Kivule na kazi yake ni fundi selemala,mwingine ni Maulid Mohamed Mzungu maarufu kwa jina la Mbonde (54) mkazi wa Kisevule ambaye kazi yake ni mkulima.

Amewataja watuhumiwa wengine ni John Andrew John (40) mkazi wa Magore-Kitunda ambaye ni mfanyabiashara na amekuwa na jukumu la kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka kituo cha Soka Kambiasso, Pia wanamshikilia Seleman Matola Said(24) mkazi wa Temeke –Wailes Matola ni mtoto wa dada yake na mtuhumiwa Alhaj Kambi.

Mwingine ni Hussein Mohamed Pazi(41) mkazi wa Kibugumo wilayani Kigamboni ambaye ni mfanyabiashara na mtuhumiwa wa tisa ni Ramadhan Rashid Chalamila(27)ambaye ni mfanyabiashara. “Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad