Moja kati ya kauli inayowaumiza mashabiki wengi wa Yanga ni ile ya Rais wa klabu hiyo Eng. Heris Said @caamil_88 kudai kuwa 'eti kuna mashabiki wa @Yangasc wala mihogo wanaumia na timu kuliko viongozi.
Suala sio mashabiki wa Yanga, ila 'wala mihogo' hii kauli sio sawa kwa mashabiki hasa wenye timu yao.
Viongozi wengi ndani ya Yanga wameajiriwa, hivyo kuna wakati wataondoka na kuwaacha mashabiki wakiwa pale pale.
Heris Saidi anadai mdhamini wa timu hiyo bwana Ghalib anaumia na timu na kuna wakati anakosa kabisa usingizi kwa ajili ya timu, lakini akumbuke wapo mashabiki wanaopoteza fahamu uwanjani baada ya matokeo mabaya, wapo wanatoka uwanjani wakiwa wanalia, sijui kama Gharib amewahi hata kulia.
Siku zote msingi wa timu ni mashabiki, klabu ya Liverpool pale Uingereza wana msemo wao unasema 'You Will Never Walk Alone' walikuwa na maana kubwa sana hasa timu inahitaji mashabiki.
Injinia anatakiwa kujua hao wala mihogo wa Chanika ndio wanaonunua jezi za klabu ya Yanga kwa bei Tsh. 35,000 kwasababu tu ina nembo ya klabu yao, wakati fedha hizo anaweza kwenda kununua T-shirt tatu za elfu 10, na chenji inabaki, lakini anakwenda kununua jezi yenye nembo ya Yanga, wanastahili kupewa heshima yao.
Leo hii ikiwaambia wachangie klabu wapo tayari waweke mihogo pembeni na kuchukua 1000 yao kuchangia klabu, kwa nini wadharauliwe watu wanaosapoti timu yao?
Unahitaji wala mihogo hao hao waujaze Uwanja wa Mkapa kusapoti timu yao, basi watafutie jina la kuwaita na sio wala Mihogo, inaonesha kuwadharau.
Furaha ya mashabiki ni kuona timu waliovaa jezi yao inashinda, wanatakiwa kuheshimiwa sio kuwaudhi, wala mihogo sio jina zuri kuwaita.
@badimchomolo