Kidomo Domo Champonza Christian Ronald Kupigwa Fine ya Mabilioni


Kufuatia mahojiano ya mshambuliaji nyota wa klabu ya Manchester United, Cristiano Ronaldo na mtangazaji nguli wa gazeti la The Sun, Uingereza, Piers Morgan ambayo yameibua hisia mseto, klabu ya Man United inatajwa kumpiga faini nyota wake huyo.

Mahojiano hayo ambayo yanatajwa yatatoka rasmi kuanzia kesho, sasa tovuti mbalimbali Uingereza ikiwemo ya Metro imeripoti kuwa Cristiano Ronaldo atakumbwa na faini ya £1m ambayo ni sawa na Bilioni 2.7 za Kitanzania.

Fahamu, kwenye sehemu ya mahojiano hayo, Ronaldo ameeleza mengi ikiwemo kuhisi kusalitiwa kwenye klabu, na kueleza baadhi ya watu ndani ya klabu hiyo kutomuhitaji.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad