Ndoto za wasanii wengi ni kuwa na maisha mazuri na yale ya kifahari. Sio tu kwa wasanii, ila kwa watu wengi.
Wasanii na mastaa wana aina ya maisha yao ya kipekee, kuwa na magari mazuri (Ndinga kali), Nyumba za maana. Hapo kwenye nyumba sasa, wanataka iwe na kila kitu kama vile bwawa la kuogelea (Swimming Pool).
Ndio mambo ya kisasa, lakini umakini unatakiwa hapa hasa kwenye bwawa la kuogelea. Kwao sio tatizo, lakini shida inakuja kwa watoto wenye umri mdogo.
mazingira ya mabwawa hayo sio rafiki kwa watoto, hivyo ujikuta wanapoteza watoto wao kwa kuzama na maji.
2018 msanii wa muziki nchini Nigeria, D'Banj alimpoteza mtoto wake wa mwaka mmoja na mwezi yaani alikuwa na miezi 13, alifariki kwa kuzama kwenye bwawa la nyumbani kwao.
Wakati huo D'Banj alikuwa Los Angeles, Marekani kwenye tuzo za BET, huku akiwa na furaha kuwania tuzo hizo kubwa Marekani ghafla anapigiwa simu mtoto wako amekutwa amefariki kwenye bwala la kuogelea. Hakuwa na furaha tena, ila alijuta kwanini hakuweka uzio.
Jana msanii Davido naye alitangaza kifo cha mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 3 kilichotokea nyumbani kwake kwa kuzama kwenye bwala la kuogelea. Inauma sana, bwala lako kwa ajili ya starehe lakini unakuja kumpoteza mtoto wako kipenzi.
Juzi tu hapa, alitoka kumfanyia sherehe ya kutimiza miaka 3 ya kuzaliwa kwake. Hapa kuna kitu cha kujifunza kwa mastaa hata mtu mwenye ndoto za kutaka kujenga nyumba ambayo itakuwa na bwawa la kuogelea, unapaswa kuweka uzio au kingo kwa watoto.
Pole kwa Davido, D'Banj na wengine ambao wamepoteza wapendwa wao kwenye bwawa la kuogelea.