Kisa Waarabu… Aziz Ki, Mayele Waapa Kuwamaliza Club Africain Nchini Tunisia





KUELEKEA mchezo wa marudiano dhidi ya Club Africain ya Tunisia, uongozi wa Yanga umeibuka na kuweka wazi kuwa mastaa wa timu hiyo wamesikia malalamiko ya mashabiki wao na kuapa kuyachukua kama motisha kuhakikisha wanawashangaza watu kwenye mchezo wa marudiano nchini Tunisia.

 

Yanga Jumatano wiki hii wakiwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar walilazimishwa suluhu na wageni wao Club Africain katika mchezo wa kwanza wa wa mtoano Kombe la Shirikisho Afrika na kuzua malalamiko makubwa kwa wadau mbalimbali wa soka hususani mashabiki wa Yanga.



Yanga watarudiana na wapinzani wao hao Novemba 9, huu nchini Tunisia, ambapo mshindi wa jumla wa michezo hiyo atafuzu hatua ya makundi.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe alisema: “Kama taasisi ambayo ina malengo makubwa tumesikitishwa sana na matokeo ambayo tumeyapata juzi Jumatano, wachezaji na viongozi kwa pamoja wamesikia maumivu ya mashabiki na wanachama wetu na kila mmoja ameapa kutimiza wajibu wake kwa asilimia 100 ili kuhakikisha tunapata matokeo yatakayotupeleka makundi nchini Tunisia.

 

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini tunaamini inawezekana na tutapambana kwa jasho na damu kuhakikisha tunafuzu.”

Stori: Joel Thomas

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad