"Mwanangu Majaliwa ni mwanangu wa pili nina watoto watano ambao naishi nao hapa mtaa wa Nyamkazi, kwa wakati huu nina umri wa miaka 47 shughuli zangu ni busness tu za kuuza kile kale ili niweze kupata rizki, Majaliwa mwanangu sasa hivi ana miaka 20 na kazi yake kubwa alikuwa anaimba.
Wakati napata taarifa za agizo la Rais Samia Suluhu kumzawadia mwanangu kazi nilikuwa kijijini kwaajili ya kutafuta rizki, nilivyofika nyumbani nilikuta amevimba jicho na mkono nilipomuuliza kwanini amevimba akanijibu "mama nilikuwa najitahidi kuzama kwenye maji kutafuta jinsi ya kumuokoa Rubani" nikasema mbona wewe siyo mzoefu wa maji? akasema mama mimi ni mzoefu wa maji pengine natorokaga naenda kuogelea kwenye kaziwa basi nikawa nacheka tu.
Maisha ya majaliwa nayaendesha mimi kama mimi mama yao isipokuwa baba yake hayupo kwa wakati huu yuko mbali nasi hatuishi nae, ujasiri wa Majaliwa haujaanza leo, Zamani akiwa mdogo amewahi kwenda kanisani kwa Waromani akaenda mpaka madhabahuni jambo lililowashangaza sana watu kwa ujasiri ule.
"Sasa nimefurahi sana na ninashukuru sana kutendo hicho cha kumsaidia siyo kiasi cha pesa tu wamempa hadi ajira ili aweze kuwasaidia ndugu zake na mimi kama mama yake na jamii ambao watakao weza kuwa karibu naye kwa upendo lakini". credit DjMix FB!