Mashabiki Kulindwa na Teknolojia QATAR



Katika kuhakikishaUlinzi na Usalama kwa Mashabiki watakaoshuhudia Fainali za Kombe la Dunia, Serikali ya nchini QATAR kupitia kamati kuu ya Maandalizi imeandaa chumba maalum kitakachokua na teknolojia ya kufuatia matukio yote hatua kwa hatua.


Fainali hizo zimepangwa kuanza Jumapili (Novemba 20) kwa wenyeji QATAR kupapatuana na Ecuador mjini Al Khor katika Uwanja wa Al Bayt.


Chumba hicho Maalum kipo mjini Doha, ambacho kina mamia ya Luninga ‘TV’ ambazo zitaonyesha umati wote wa watu watakaohudhuria michezo ya Fainali za Kombe la Dunia 2022.


Qatar imeweka Kitengo Maalumu cha teknolojia ambacho kitatumia “akili bandia” (artificial intelligence) kuwafuatilia Mashabiki, kutabiri kuongezeka kwa umati na kudhibiti jotoridi viwanjani.


Chumba hicho kitakuwa na zaidi ya mafundi 100 watakaofanya kazi saa 24, wakifuatilia camera 22,000 za usalama kupitia vitengo 200,000 vilivyoungwa kwa teknolojia.


Hapo ndipo mageti yatafunguliwa na kufungwa, upatikanaji wa maji safi na viyoyozi vitafuatiliwa.


Kwa kubonyeza kitufe kimoja tu maafisa husika wataweza kutoka kufuatilia uwanja mmoja kwenda uwanja mwingine.


Wataalamu wa Usalama wa mitandaoni na wa ugaidi, usafiri/uchukuzi watakuwemo pamoja na maafisa wengine wa Qatar na FIFA.


Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Hamad Ahmed al-Mohannadi ameeleza kuwa dhana hii ya kuviunganisha Viwanja kiteknolojia ni ya kwanza ya aina yake kutumika katika Kombe la Dunia.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad