Shirikisho la Soka Duniani FIFA na Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia 2022 ‘QATAR’ wameandaa taratibu zikatazotumika viwanjani wakati wa Fainali hizo zilizoanza jana Jumapili (Novemba 20), ambazo ni ngumu kuliko miaka ya nyuma.
Mashabiki waliokwenda QATAR kwa ajili ya kuzishangilia timu za Mataifa yao wametakiwa kuvaa vizuri na kujisitiri haswa maeneo nyeti ya miili yao, pia wameaswa kuwa michoro ya mwilini yani ‘Tattoo’ haitakiwi kuonekana maana ile sio nguo.
Kingine ni kuwa mtu yotote atakayeingia kutizama michezo ya Fainali hizo asiwe kalewa pombe au dawa za kulevya, hili ni kosa kisheria kwa nchi ya QATAR.
Chupa, vikombe, makopo au vitu vyovyote vinavyoweza kurushwa na kuumiza mtu haviruhusiwi viwanjani, pia vyakula vya aina zote haviruhusiwi labda tu awe amebebewa mtoto.
Vuvuzela zimepigwa marufuku na vitu vingine kama maputo havitoruhusiwa.
Taratibu zimeanza kutumia tangu jana Jumapili (Novemba 20) wakati wa mchezo wa Ufunguzi kati ya Wenyeji QATAR ambao walikubali kuchapwa Bakora 2-0 dhidi ya Ecuador.