MASHABIKI WANA HAKI YA KUMLAUMU NABI?
Kwenye mchezo dhidi ya Club Africain, Yanga hawakuwa na lolote, walicheza kama wapo ugenini, ninaamini wapinzani walifurahi levo ya uchezaji wa Yanga kwa kuwa hakuwa na madhara kwao.
Yanga walicheza taratibu sana (Slow), kama wameshtukizwa kwenye mchezo huo muhimu, walikosa ubunifu kabisa.
Makosa yalianzia kwa kocha Nabi mwenyewe kwa aina ya upangaji wa kikosi chake. Kuanza na Yanick Bangala kwenye eneo la ulinzi wa kati pamoja na Dickson Job badala ya Mwamnyeto na Job.
Shida ilianzia hapa, kwa nini?
Yanga ilikuwa haitakiwi kujilinda sana, ilitakiwa kuingia na mfumo wa kushambulia tangu dakika 15 za kwanza, Bangala alitakiwa kucheza namba sita ili kuwalinda walinzi na kutengeneza connection kati ya walinzi na viungo washambuliaji, Kharid Aucho hakuweza kufanya hivyo.
Feisal Toto hakuonekana kabisa kwasababu alikosa connection kutoka kwa Bangala.
Kuanza na Tuisila Kisinda haikuwa sawa. Ubora wa Kisinda haujawa bora tangu aliporejea Tanzania, alionekana kukosa fitness, nafasi yake alipaswa kuanza na Faridi Mussa mwenye uwezo wa kushambulia na kukaba.
Faridi mbali na kuwa na kasi, lakini ana uwezo wa kutengeneza mashambulizi, kumiliki mpira na kuongeza nguvu eneo la katikati.
Bado hakuna ubora mkubwa ambao unaweza kuupata kwa kuwatumia wachezaji wawili kwa pamoja wenye kucheza namba 10, Feisali na Aziz Ki.
Nabi anatakiwa kukubali kuanza na mmoja kati yao ili aweze kukupa ubora wake. Kutokana na hali hiyo mashabiki wana kila sababu ya kumtupia lawama Nabi.
Club Africain walifanya kile watakacho wakiwa ugenini, walipooza mashambulizi, walipoteza muda hadi dakika 90 zikamalizika kwa Mkapa, zimebaki zingine kule Tunisia tarehe 9.
Kwa hali ya kawaida Yanga hawana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano, lakini kwenye makaratasi bado ni 50 kwa 50. Nabi ana nafasi ya kupunguza lawama, lakini kwa sasa acha alaumiwe.
Cc @badimchomolo