Mdau "Laana ya Kudharau Tuzo za Nyumbani Inamtesa Diamond Platnumz"


Baada ya msanii tokea nchini Uganda, @eddykenzo kuwa nominated kwenye tuzo za Grammy na kuweka rekodi kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki ya kuwa msanii wa kwanza kutajwa kuwania tuzo hizo kubwa ulimwenguni, wengi wamereact na kila mmoja akiongea lake, lakini maoni mengi yakibeza juhudi za mwanamuziki #Diamondplatnumz ambaye kwenye mahojiano na #Grammy mwaka 2020 alidai siku akitajwa kuwania ama kushinda tuzo hiyo basi atafanya show ya bure kwenye stadium kwa siku 3 mfululizo na kuiweka hadharani tuzo hiyo kila shabiki aione ama kuigusa maana wao ndio watakuwa wamefanikisha hilo kutokea.

Kuna mdau kaenda mbali zaidi na kudai kitendo cha Diamond kudharau tuzo za Nyumbani (TMA) ni laana tosha, na hasipo tubu basi Grammy atazisikia kwa majirani. Je, mdau yuko sahihi, ni kweli hakuna watu walizikataa tuzo flani na wakapata tuzo kubwa zaidi ya hizo? Au neno nyumbani ndilo kubwa zaidi? Majibu baki nayo.

Eddy Kenzo ni moja ya wasanii wazuri ambao wako Underrated kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki hasa linapokuja suala la Diamond, na hii imejitokeza mara nyingi msanii huyo anapokutana na aina ya wasanii kama Diamond kwenye vipengere vya tuzo kama #Afrima, #afrimma n.k japo kabeba tuzo kadhaa mbele ya Diamond.

Ukumbuke tu, Eddy ndiye msanii wa kwanza kutunzwa tuzo ya BET kwa Afrika Mashariki, Mwaka 2015 kabla #Rayvanny hajainyakua tuzo hiyo mwaka 2017, Eddy Kenzo ndiye msanii wa kwanza toka Afrika Mashariki kuingia kwenye chart za BILLBOARD US AFROBEATS (Nyimbo za Afrika zinazo fanya vizuri zaidi nchini Marekani) kupitia wimbo wa Gimmie Love ambao ndio uliochaguliwa kwenye Grammy. Uwenda Muziki wa Eddy Kenzo pia ukawa hauna nguvu sana Afrika Mashariki sehemu ambayo kwasasa tunaona ili kutoboa lazima uimbe amapiano, au Kinigeria flani n.k,

Kuna la kujifunza hapa, Chukueni Notes kwa Eddy Kenzo namna ya kuwa star mkubwa bila kelele.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad