Watu wanne akiwemo raia Burundi wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa tuhuma za kumvamia na kumuua kwa kumchinja shingo kwa panga, mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina la Tegemeo Rashid, Mkazi wa Kata ya Buziku wilayani Chato mkoani humo, huku majirani wa mfanyabiashara huyo wakidai kunusurika kifo baada ya kufyatuliwa risasi na majambazi hao walipojaribu kumsaidia Rashid.
.
Baada ya mauaji hayo Jeshi la Polisi liliendesha msako wa mtaa kwa mtaa na kuwakamata majambazi hao wakiwa na silaha ya kivita aina ya AK-47 ikiwa imefukiwa shambani.