Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya ndege Mussa Mbura amethibitisha taarifa zilizotolewa na Mbunge Neema Lugandira kuhusu ndege ya Air Tanzania kushindwa kutua Bukoba Airport na kusema chanzo ni mvua kuleta ukungu na kusema sio Bukoba pekee hata Mpanda ndege zimeshindwa kutua kwasababu ya hali ya hewa kuwa mbaya.
"Haya mambo ya ndege kutotua kwenye kiwanja fulani kwasababu ya hali ya hewa hayajatokea tu Bukoba, ndege zilizokuwa zinaenda Mpanda leo zimesitisha safari kwasababu ya hali ya hewa, mvua ni nyingi na zinasababisha ukungu na Marubani kutokuona viwanja kwa urahisi, kwahiyo sababu ya msingi ya ndege kutokutua Bukoba leo ni hali ya hewa hasa mvua"
"Kwahiyo ishu sio eneo (kiwanja Bukoba) ishu ni hali ya hewa, kwahiyo sababu za kusema labda twende kiwanja kingine tulisema mwanzo litaangaliwa kitaalamu na itategemea na uwezo wa Serikali kibajeti kujenga uwanja mpya ni gharama kubwa Serikali ikiona bajeti ipo basi taratibu zitaendelea lakini tunasema kusitishwa kwa safari hizi chanzo sio kwasababu uwanja mwingine haupo hata uwanja mwingine ungekuwepo bado hali ya hewa ya Bukoba ipo ambavyo ipo"