Nay wa Mitego Adaiwa Kuwa Mafichoni Baada ya Kutoa Wimbo Wenye Utata Mwingi




Kama kuna kitu kimoja ambacho wasanii kutoka Tanzania wamekikumbatia basi ni weledi wa kujieleza kupitia muziki.

Wasanii wengi hutumia biti za muziki na kuingiza maneno yao ya hisia ambayo yanabeba ujumbe wao na hisia zao kwa njia inayosogeza pakubwa, kumfanya yeyote anayesikiliza kukubali kazi hiyo.

Msanii Nay wa Mitego, ambaye ni mmoja wa marapa wakubwa zaidi nchini humo wiki moja iliyopita aliachia kibao kimoja cha kiharakati vile, kibao ambacho kimemzushia ukakasi baina yake na uongozi wa taifa hilo.

Taarifa mbali mbali, japo hazijadhibitishwa zinahoji kwamba msanii huyo yupo mafichoni kwa kuhofia vyombo ya dola

Lakini je, nini maudhui ya wimbo huo? Usijali, maelezo kamili haya hapa!

Nay wa Mitego wiki jana aliachia wimbo kwa jina ‘Sauti ya Watu’, wimbo wenye maudhui ya kuusimanga uongozi wa taifa kwa kuwanyanyasa walala hoi kiuchumi huku wenye nacho wakizidi kujilimbikizia.


Katika wimbo huo ambao tayari umezua ukakasi mtanange, Nay anatoa mzomo mkali kwa serikali ya rais mama Samia Suluhu Hassan hata kama anaanza kwa kumuomba radhi kutokana na kwamba alijua atamkwaza katika ujumbe kwenye wimbo huo.

“Hii sio sauti ya kiharakati, wala ukombozi wa Musa na fimbo yake, bali haya ni maumivu ya mnyonge, anayewakilisha walala hoi wenzake, kwenye kinywa kilichokosa pa kusemea hisia zake. Rais natanguliza samahani kwa wale nitakaowakwaza, yamenifika kwenye koo nimeshindwa kunyamaza,” Nay wa Mitego anaanza kwa uchachu mno.


Kwa weledi wa aina yake, rapa huyo anayaweka maneno yake makali kwa njia ya kishairi huku akisema kwamba wafisadi waliotumbuliwa katika serikali ya hayati Magufuli wamesharudishwa kazini ambapo mradi wa milioni moja wanautaja kuwa wa mabilioni.

“Kilio cha kila mtu pesa hakuna imefichwa wapi, siku hizi mpaka vigenge vya nyanya TRA inataka kodi. Maskini amejichanga vipesa benki anakatwa tozo. Hizo V8 mnazonunua si hela zetu za kodi? Naona mnafurahia kuliko hata walipa kodi. Mnajenga hospitali, dawa hakuna, mnatujengea shule lakini walimu hatuna,” Nay True Boy alizidi kugongelea misumari kwenye jeneza.

Isitoshe, aliwaingilia wanasiasa wanawaambia vijana kujiajiri wakati wao wenyewe tayari wametafuta ajira kwa wananchi ili kuchaguliwa kwa nyadhifa za kisiasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad