Nchi iliyopeleka wachezaji kwenye Kombe la Dunia wakisindikizwa na ndege za kivita



Miongoni mwa timu zinazocheza leo kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar ni pamoja na timu ya taifa ya Poland ambayo ilivutia vyombo vya habari vya kimataifa ilipoondoka nchini mwao.

Bado kuna gumzo kuhusu jinsi ulimwengu ulivyoshangazwa na namna Timu ya Taifa ya Poland ilivyoondoka nchini mwao walipokuwa wakielekea katika jiji la Dosha nchini Qatar, kushiriki Kombe la Dunia.

Ndege iliyowabeba wachezaji wa Poland walioruka siku ya Alhamisi ilionekana ikiwa katikati ya ndege za kivita za F-16.

Ukurasa rasmi wa timu ya Poland kwenye Twitter ulichapisha video ya ndege za F-16 zikifuata ndege ya kiraia ambayo wachezaji walikuwa wamepanda.


"Tulipelekwa hadi kusini mwa Poland tukiwa na ndege za kivita za  F-16," iliandikwa kwenye video hiyo.

Katika video hiyo hiyo, nukuu pia iliandikwa kuwashukuru marubani wa kijeshi wa Poland waliochukua hatua hiyo.


Chanzo cha picha, LACZYNASPILKA

Picha zilizotolewa pia zilionyesha mmoja wa marubani wa ndege ya F-16 akiwa na nembo ya timu ya taifa ya Poland kwenye dirisha.


Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya watu wawili kuuawa na kombora lisilojulikana lililoanguka huko Poland, wakati wa vita kati ya Urusi na Ukraine.

Tangu shambulio hilo, jeshi la Poland limekuwa katika hali ya tahadhari. Vyombo vya habari vya Poland vilitangaza hatua iliyochukuliwa na jeshi kutetea timu ya taifa iliyosafiri hadi Qatar.

Kumbe la Dunia Qatar
Timu ya Poland itacheza na timu ya Mexico kutoka Amerika Kusini jioni ya leo, saa 7:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Siku nne baadaye Poland itacheza dhidi ya Saudi Arabia katika kundi moja.

Poland ni moja ya timu bora katika Kundi C, ambalo pia linajumuisha Argentina.

Mechi ya mwisho katika kundi hilo itakuwa kati ya Poland na Argentina tarehe 30 mwezi huu.

Nyota wa Barcelona, ​​Robert Lewandowski na wachezaji wenzake wanataka kuipeleka timu yao katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia, na iwapo watashinda itakuwa ni mara ya kwanza kufika hatua hiyo tangu mwaka 1986.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad