Hauko peke yako – Meridianbet ina ujumbe mzito kwa wanawake wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinsia.
Popote ulipo, mtaani, maeneo ya kazi, maeneo binafsi…
Wanawake wanne kati ya watano hupitia ukatili mitaani. Mmoja kati ya wanawake watatu huathiriwa na ukatili wa kijinsia na kimwili. Mmoja kati ya wanawake watano amepitia unyanyasaji mtandaoni, lakini pia aslimia 50 ya wanawake wamepitia unyanyasaji wa kimwilini maeneo yao ya kazi! Ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake hujidhihirisha kwa njia na aina mbalimbali, sio ya kimwili tu.
Pinga Ukatili dhidi ya Wanawake!
Meridianbet wamekuwa wamekuwa wakifanya kazi kwa miaka mingi kupaza sauti kuhusu swala hili ili kupinga ukatili dhidi ya wanawake na kuongeza ufahamu wa umuhimu wa kupambana na ukatili bila kusubiri tatizo linapotokea.
Kampuni imedhihirisha azma yake ya kushiriki kikamilifu kama kampuni inayowajibika kwa jamii kwa zaidi ya miongo miwili, ikikazia umuhimu wa usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake, na kutovumilia kwa aina yoyote ya unyanyasaji au ubaguzi kupitia mfano wake na mfumo wa biashara.
Wanawake Wanaosimamia Meridianbet
Kama kampuni iliyojikita katika teknolojia, tunataka kuwa kitovu cha vipaji na mwajiri wa chaguo kwa wote, bila ubaguzi wa aina yoyote.
Wanawake wanachangia zaidi ya asilimia 55 ya usimamizi wa juu wa Meridianbet, ambao unazidi viwango vya juu zaidi vya DE&I. Idadi hii ni kubwa zaidi katika masoko ya Afrika na Ulaya, na usimamizi wa wanawake unafikia aslimia 62 na 56 mtawalia.
Wanawake wanawakilishwa sawa sawa katika sehemu zote za biashara – Rasilimali watu, masoko, usimamizi wa maduka, na utengenezaji wa programu, hiyo inaonyesha hakuna usawa wa kijinsia unaowezekana bila uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake.
Kauli mbiu hii ya Umoja wa Mataifa, inayosema “Usawa wa Kijnsia Leo kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Kesho” ni tamaduni ya Meridianbet.
Katika ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Unyanyasaji Dhidi ya Wanawake, Kampuni inakumbusha kwamba kutatua tatizo hili zito ni lazima liwe kipaumbele sio tu kazi katika mamlaka ya serikali, lakini pia katika mazingira ya biashara, ambayo yana ushawishi mkubwa katika kukuza maadili ya kweli ya kitamaduni, uvumilivu na heshima.