Precision Air "Tutazisaidia Familia Zilizo Athirika na Ajali ya Ndege"


Uongozi wa Shirika la Ndege la Precision Air kupitia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Patrick Mwanri umetoa taarifa kuhusu ajali ya Ndege yao iliyotokea Bukoba mkoani Kagera leo asubuhi wakati ikitua na kusema utazi-support Familia zilizoathirika.

“Ndege zetu nyingine zote zipo salama, iliyopata ajali ni moja tu iliyokuwa inatoka Dar es salaam kwenda Bukoba, kutakuwa na mabadiliko kidogo ya safari za ndege mchana huu na kesho kutokana na hili tatizo”

“Hadi sasa tumeshaokoa abiria 26, tulikuwa na abiria 39 (Wakubwa 38 na Mtoto mmoja) na Wafanyakazi wanne jumla ni 43”

“Niwaombe Waandishi wa Habari tupo kwenye majonzi makubwa ni vizuri tutoe taarifa sahihi ili tusipotoshe umma, Familia zilizoathirika tutahakikisha tunazipatia support inayotakiwa”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad