Sadio Mane Atajwa Safari ya QATAR Licha ya Kuumia



Mshambuliaji na Nahodha wa Kikosi cha Senegal Sadio Mane ametajwa kwenye kikosi cha mwisho cha timu hiyo, tayari kwa Fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza baadae mwezi huu nchini QATAR.


Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alizua hofu ya kucheza Fainali hizo, baada ya kuumia mguu akiwa kwenye mchezo wa Ligi ya Ujerumani Jumanne (Novemba 08) ulioshuhudia FC Bayern Munich ikishinda 6-1 dhidi ya Werder Bremen.


Kocha Mkuu wa Senegal Alioy Cisse amesema amelazimika kumuita Mane kwenye kikosi, akiwa na matarajio ya kumtumia kwenye Michezo ya Kombe la Dunia kutokana na maendeleo yake kuridhisha.


Marekani ya kwanza kuwasili QATAR

“Tunaendelea kufuatilia hali yake kwa uangalizi wa madaktari wetu, tunaamini ataweza kuwa sehemu ya kikosi katika Michezo itakayotukabili nchini QATAR,”


“Jana Alhamis , Sadio alitumia muda mwingi akiwa mjini Munich kabla ya kusafiri kwenda Austria kwa ajili ya kufanya vipimo mbadala, majibu yametupa faraja, na ndio maana nimemtaja kwenye kikosi changu.”


“Sikutaka kumuacha kwa sababu naamini ataweza kutusaidia tukiwa QATAR, ninaamini kila mmoja ataendelea kuamini hili kwa sababu Senegal inamuhitaji Mane na Mane anaihitaji Senegal kwa sasa.” amesema Alioy Cisse alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dakar leo Ijumaa (Novemba 10)


Kocha Walid Regragui ajilipua kwa Hakim Ziyec

Hata hivyo tayari Benchi la Ufundi la FC Bayern Munich limethibitisha kuwa, Mane hatokuwa sehemu ya kikosi kesho Jumamosi (Novemba 12) dhidi ya Schalke 04, baada ya kuthibitika ana majeraha ya katika mguu wake wa kulia.


Senegal itaanza Kampeni ya kusaka ubingwa wa Dunia kwa kupambana Uholanzi katika mchezo wa Kundi A, utakaopigwa Novemba 21.


Kikosi cha mwisho cha Senegal kilichotajwa leo, WALINDA LANGO: Seny Dieng (Queens Park Rangers), Alfred Gomis (Rennes), Edouard Mendy (Chelsea).


MABEKI: Fode Ballo-Toure (AC Milan), Pape Abdou Cisse (Olympiakos), Abdou Diallo (RB Leipzig), Ismail Jakobs (Monaco), Kalidou Koulibaly (Chelsea), Formose Mendy (Amiens) na Youssouf Sabaly (Real Betis).


VIUNGO: Pathe Ciss (Rayo Vallecano), Krepin Diatta (Monaco), Idrissa Gana Gueye (Everton), Pape Gueye (Marseille), Cheikhou Kouyate (Nottingham Forest), Mamadou Loum Ndiaye (Reading), Nampalys Mendy (Leicester City), Moustapha Name (Pafos) na Pape Matar Sarr (Tottenham Hotspur).


WASHAMBULIAJI: Boulaye Dia (Salernitana), Famara Diedhiou (Alanyaspor), Bamba Dieng (Marseille), Nicolas Jackson (Villarreal), Sadio Mane (Bayern Munich), Iliman Ndiaye (Sheffield United) na Ismaila Sarr (Watford).

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad