Wakazi "Serikali Acheni Mzaha, Wadau Acheni Kiki Ajali ya Bukoba, Wahuduma wa Ndege Wanastahili Pongezi"




Kwanza kabisa, Mwenyezi Mungu awarehemu Marehemu, awatie nguvu familia, na awaponye Majeruhi.

Pili pongezi kwa waokoaji (first responders) ambao wengi ni wavuvi ambao walijitoa kwa moyo kuokoa wenzao ingawa mazingira na vifaa havikuwa rafiki na pia duni (respectively).

ILA Naona tumerudi rasmi “Enzi za Mwendazake”. Badala ya ku accept mapungufu na kuwa Accountable (kuna Watu wanapaswa kujiuzulu), na kuchukua hatua ya kujenga Taasisi zetu ili makosa yasijirudie… Sisi tunamuwezesha Dogo Majaliwa na kumfanya a spectacle.

Swala la kumpa Million halina tofauti na Aliyokuwa anafanya Mwendazake, kwamba kukusadia ni mpaka akufikie Akupe papai, akupe hela, au anunue bidhaa yako.

Jengeni Taasisi Imara!! Kama mmeshindwa, pisheni watu wengine watuongoze; wenye maono na dhamira ya dhati kufanya hivyo. Cover-ups, Deflections & Ignorance sio tiba za Majanga haya ambayo Taifa letu yanaipitia. Nimeona Press conference ya Msigwa kidogo nitukane huko twitter, ridiculous!!

ALAFU WADAU PIA ACHENI KIKI!! Yanga ni timu yangu, ila na nyie acheni kutafuta KIKI kwa huyo Dogo…

Kwanza nyie ni timu ya WANANCHI, hebu onyesheni hilo kwa kusaidia “Wananchi Wote walioathirika”. Na besides there is more than one HERO (account za survivors zinasema Air Hostess were brave too)

Do something; Watu wana PTSD watahitaji Counseling, Kuna Watu wamepoteza Wazazi/Breadwinners, Kuna kachanga Kamepona ila sijui kama Wazazi wake Wamepona, etc. Kukimbilia kumpa hela huyo dogo peke yake, au kwa Rais na Serikali kumpeleka jeshi la Uokoaji sio Tiba!! DO BETTER!!

The Leader

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad