New Content Item (1)
Dodoma. Serikali imetenga nafasi 30,000 za ajira kwa kada mbalimbali katika mwaka wa 2022/23, Bunge limeelezwa leo Alhamisi.
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Novemba 10, 2022 ambapo amesema mchakato wa ajira hizo unaendelea.
Ndejembi alikuwa anajibu swali la Mbunge Viti Maalum, Asia Halamga (CCM) ambaye ametaka kujua ni lini Serikali itaajiri wataalamu wa mazingira ili kusaidia kuweka vyema mazingira.
Kuhusu wataalamu wa mazingira. Ndejembi amesema Serikali inakamilisha mchakato wa kuajiri watu 223 wa kada ya mazingira ambapo hatua zilizopo ni kwenye taasisi mbalimbali zinaendelea kukamilisha michakato yao.
Hata hivyo, Spika amehoji kwa nini ajira 213 hazijakamili na kuomba maelekezo ya kina nini tatizo hata miradi isikamilike.
"Sekretarieti ya Ajira haina shida isipokuwa taasisi za Serikali ambapo ziliomba kada hiyo lakini kuna vitu wanakamilisha ndiyo maana ya kuendelea na mchakato wa ajira hizo," amesema Ndejembi.