Serikali Yawaonya Mapasta Dhidi ya Kudai Wana Uwezo wa Kuponya Ukimwi



Baraza la Kitaifa la Kudhibiti Ugonjwa wa Kuambikizana (NSDCC), limewaonya viongozi wa kidini dhidi ya kueneza propaganda kwamba wanaweza kuponya Virusi Vya Ukimwi kupitia nguvu za Mungu.

Katika taarifa Jumapili, Oktoba 29, NSDCC ilionya umma kuhusu ya madai ya wachungaji kwamba mgonjwa wa VVU aliponywa kupitia maombi.

NSDCC lilishikilia kuwa dawa ya kutibu ugonjwa huo bado haijapatikana na kuwa kuwapotosha wafuasi wao kutasababisha maafa nchini.


"Japo tunakubali kwamba maombi ni muhimu kwa ustawi wa kiroho, kisaikolojia kwa waumini wengi, madai ambayo hayajathibitishwa ya uponyaji wa VVU kwa imani hapo awali yamesababisha kupotezwa kwa."

"Hadi sasa, hatuna tiba iliyothibitishwa ambayo inaweza kusimamiwa katika kituo cha afya cha umma," taarifa hiyo ilisoma kwa sehemu.

Baraza hilo lilizua wasiwasi kuwa madai hayo potovu yanaweza kuathiri utumizi wa dawa za kurefusha maisha kwa wagonjwa na hivyo kuhujumu hatua zilizopigwa a serikali katika kudhibiti ugonjwa huo.

"Kutatizika kwa matibabu ya VVU kuna matokeo mabaya ikiwa ni pamoja na uharibifu wa viungo vya mwili ambao hauwezi kurekebishwa," NSDCC ilieleza.

NSDCC lilitoa wito kwa viongozi wa kidini kuongoza kondoo wao kwa kushughulikia matatizo ya kijamii na kitamaduni ambayo watu walioambukizwa wanakabiliwa nayo ili kupiga jeki vita dhidi ya ugonjwa huo hatari.


"Tunawaomba jamii ya kidini kufanya kazi kwa karibu na waumini na washirika wengine ili kutokomeza unyanyapaa unaohusiana na ubaguzi ambao unaendelea kupuuza mafanikio yaliyopatikana katika vita vya VVU," shirika lilisema.

Taarifa ya NSDCC inajiri siku chache baada ya kusambaa kwa habari za mwanamume mmoja ambaye alikuwa na VVU alipimwa na kuthibitishwa kwamba amepona virusi hivyo baada ya maombi.



Mnamo Agosti, Wizara ya Afya ilitangaza kwamba maambukizi ya VVU nchini yalikuwa yamepungua.

Hata hivyo, ilizua wasiwasi kufuatia kuongezeka kwa maambukizo mapya miongoni mwa vijana.

Ripoti ya WHO mnamo Julai 2022, ilionyesha kote duniani kulikuwa na maambukizi mapya 4000 ya Ukimwi kila siku mwaka wa 2021 miongoni mwa vijana hususan wanaotumia dawa za kulevya, wafanyabiashara wa ngono, wanaume wanaofanya ngono na wanaume, wafungwa na watu waliobadili jinsia.

Vile vile kulikuwa na jumla ya maambukizi 1.5 milioni mwaka 2021 sawa na 2020.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad