Sheria ya Kutokuvua Jezi Kwa Wachezaji Uwanjani ilianzia Hapa




Umeshawahi kuona mchezaji anaoneshwa kadi ya njano kwa kosa la kushangilia bao?

Basi tatizo lilianzia kwenye picha hiyo hapo.

Huyo ni Brandi Chastain, na hapo kwenye kwenye fainali ya Kombe la Dunia la wanawake mwaka 1999.

Chastain alikuwa nyota wa timu ya taifa ya Marekani ambayo siku hiyo ilikuwa ilicheza na China kwenye fainali.

Baada ya sare tasa dakika 120, mikwaju ya penati ikahusika.

Matokeo yakiwa 4-4, huku China wamekosa penati moja, dada huyu akafunga penati ya ushindi kwa Marekani na akashangilia kwa kuvua jezi yake kama anavyoonekana kwenye hiyo picha.

Yakaibuka malalamiko kutoka taasisi mbalimbali za maadili na makundi ya kidini kwamba haikuwa sawa kwa mtoto wa kike kuonekana dunia nzima akiwa katika hali kama ile.

Presha ikawa kubwa na Bodi ya Kimataifa Kutunga Sheria za Soka (IFAB) ikaja na sheria ya kupiga marufuku wachezaji wanawake kuvua jezi wakati wakishangilia.

Sheria hiyo ikawaibua wapigania haki sawa kwa wote wakisema haipaswi kuwa na sheria za kubagua watu kwenye soka, mchezo ambao ni wa wote.

Presha ikawa kubwa kwa mara nyingine na mwaka 2004 FIFA ikapiga marufuku hadi wachezaji wanaume kuvua jezi.

Adhabu ya kosa hili ikawa kadi ya njano, na sheria hiyo inaendelea hadi sasa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad