Twitter kuanza kuwatoza pesa watumiaji wake kwa ajili ya kupata Verification Tick. Siku chache baada ya Elon Musk kuununua mtandao huo wa Kijamii, mpango mpya ambao unatakiwa kuanza kutekelezwa mara moja ni huu ambapo mtumiaji atalazimika kulipia ($20) takribani TSh. Elfu 46 kwa mwezi.
Kwa kiasi hicho, mtumiaji atalazimika kufanya Subscription ya Twitter Blue na ndipo atapatiwa Blue Tick. Kwa wale ambao tayari wamekuwa verified tangu zamani, watalazimika kuendana na utaratibu huo mpya ndani ya siku 90. Ambapo wametakiwa kufanya Subscription ya Twitter Blue, vinginevyo watapatoeza verification badge zao.
Wafanyakazi wa Twitter wametakiwa kukamilisha mpango huo (feature) hadi kufikia November 7, la sivyo watapoteza Kazi. Twitter Blue ni feature ambayo inamuwezesha mtumiaji kupata Exclusive Access ya Premium features.