Aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Mbunge wa Bukoba Vijijini mwaka 2005-2010 Naziri Karamagi ameibuka kidedea ametangazwa kuwa mshindi katika nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera baada ya kupata asilimia 58 ya kura zote zilizopigwa
Karamagi amemshinda mwenyekiti anayemaliza muda wake, Costansia Buhiye aliyedumu katika nafasi hiyo kwa miaka 15.
Buhiye ameambulia asilimia 32 tu ya kura zilizopigwa.
Spika wa Tulia Ackson ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi ametangaa kuwa Karamagi amepata kura 669, Costansia Buhiye kura 452 Medard Mushobozi kura 18 na Novath Kwama kura Tano pekee.
Aidha ametangaza mshindi wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kareem Amri ambaye amepata kura 751 baada ya kumshinda Wilbroad Mtabuzi ambaye amepata kura 368 na Amani Kajuna kura 14.