UPDATES: Hadi Sasa Wameokolewa Watu 26 Kati ya 43 Katika Ajali ya Ndege Precision Air



Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert
Chalamila amesema Ndege ya Precision Air iliyopata ajali wakati wa kutua Bukoba leo ilikuwa imebeba Watu 43 ambapo hadi sasa wameokolewa 26 tu na kupelekwa hospital ya Rufaa ya mkoa Kagera.

Japo Mkuu wa Mkoa hajasema Watu hao waliokolewa vipi na muda gani, Mashuhuda wanasema huenda waliokolewa sekunde chache baada ya ajali kabla sehemu kubwa ya Ndege hiyo kufunikwa na maji, tunaendelea kufuatilia zaidi ili kupata taarifa kamili kutoka kwa Mamlaka.

Kwa upande mwingine RC Chalamila amewaomba Wananchi kuendelea kuwa watulivu maana mawasiliano na Marubani walioko ndani ya ndege bado yanaendelea.

Ndege hiyo ni ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF ambayo ilikua ikitokea Dar es salaam kuelekea Bukoba na ilikua na safari ya kurudi Dar es salaam kupitia Mwanza. #MillardAyoBREAKING
View all 245 comments
hawa_lifestylee Aiseeeee

14 MINUTES AGO
Photo

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad