Watu 9 akiwemo Mpishi wa Mtoto wa Staa @davido na #Chioma #Ifeanyi ambae amefariki katika Swimming pool ya Nyumbani huko Lagos wanashikiliwa na Polisi katika Jimbo la Lagos kwa sababu ya kifo cha Mtoto huyo.
Mtoto wa Staa huyo mkubwa Afrika #Ifeanyi (03) Alifariki katika Swimming pool la nyumbani katika kisiwa cha Banana Lagos Oktoba 31, 2022 siku ya Jana, inasemekana Wazazi wake #Davido na #Chioma hawakuwa Nyumbani walikuwa kwenye ziara.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja Nchini Nigeria Takriban watu tisa akiwemo Mpishi wamekamatwa baada ya kifo cha mtoto huyo kutokana na Uzembe uliofanyika mpaka mtoto akazama kwenye Bwawa hilo.