Wahudumu wapiga pesa za wagonjwa feki wa VVU



TAKUKURU mkoa wa Tanga imewabaini watumishi wa afya katika wilaya ya Muheza waliohusika kusajili wagonjwa hewa 313 wa virusi vya Ukimwi (VVU)  ili kuonyesha takwimu zipo juu za wanaoishi na VVU kwa maslahi yao binafsi ikiwemo kujinufaisha na fedha zinazotolewa na shirika la afya la AMREF. 

Awali akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake,  Kamanda wa TAKUKURU mkoa Tanga Zainabu Bakari, amesema walibaini udanganyifu huo baada ya uchunguzi na kugundua watoa huduma za afya wilayani Muheza wanahusika na kusajili majina hewa ya wagonjwa wa Virusi vya Ukimwi ili kuzidisha takwimu za ugonjwa huo kwa maslahi yao binafsi.

Alisema wahudumu wa afya wanaohusika na zoezi la kusajili na kuwafuatilia watu wanaoishi na VVU wilayani humo, wamekuwa wakilipwa posho ya gharama ya usafiri na mawasiliano  kiasi cha sh. 20,000 kwa siku kila wanapowatembelea wagonjwa hao.

Aidha amesema idadi hiyo ya wagonjwa iliondolewa kwenye mifumo na wahusika waliohusika na usajili wa wagonjwa hewa walipewa barua na kujieleza kwa kitendo cha kusajili wagonjwa hewa ambapo Wizara ya Afya imetoa maelekezo ya kufanya uhakiki kwa wateja wanaotumia dawa ambao sio halisi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad