Watuhumiwa saba kesi ya mauaji bondia Mashali waachiwa huru



Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewafutia kesi ya mauaji na kuwaachia huru, watu saba waliyokuwa wakabiliwa shtaka la kumuua bondia wa ngumi za kulipwa Tanzania, Thomas Mashali, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuieleza Mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao.

Uamuzi wa kuwafutia kesi washtakiwa hao umetolewa leo, Novemba 9, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, baada ya Wakili wa Serikali Nancy Mushimbusi, kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Washtakiwa hao ni Issa Swadaka (29), Ramadhani Ally (27), Athumani Ramadhani, Cherles Maningi (26), Mohamed Kyamba, Joseph Job na Emmanuel Michael.

Kwa kawaida kesi ya mauaji husikiliwa Katika Mahakama Kuu, lakini kesi hii imesikilizwa katika ya mkoa ambapo hakimu anayesikiliza shauri la mauaji hupewa mamlaka ya ziada kusikilizwa kesi inayosikilizwa na Mahakama Kuu.


Washtakiwa hao walishtakiwa mwaka 2016 kwa kosa moja la mauaji ya bondi, Thomas Mashali.

Kwa maana hiyo, washtakiwa wamekaa gerezani kwa muda wa miaka 7 hadi leo walipoachiwa huru.

Washtakiwa hao wamefutiwa mashtaka hayo chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai  ( CPA), sura ya 20 , iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.


Hakimu Ruboroga amesema kutokana na hati hiyo kuwasilishwa chini ya kifungu hicho, ana waachia huru washitakiwa hao, kwa sababu Jamhuri hawana nia ya kuendelea na kesi dhidi yao.

" Jamhuri( upande wa mashtaka)  hawana nia ya kuendelea dhidi yanu hiyo, Mahakama hii inawaachia huru washtakiwa wote" amedai hakimu Ruboroga.

Washtakiwa hao baada ya Hakimu Ruboroga kutamka kuwa amewafutia kesi yao,  waliangua kilio ndani ya chumba cha Mahakama hiyo huku wakipiga magoti.

Kabla ya kuwafutia kesi hiyo, Wakili Mushimbusi ameieleza Mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ililetwa kwa ajili ya  kusikilizwa, lakini DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo mahakamani hapo.


Katika kesi ya msingi, inadaiwa kuwa Oktoba 31, 2016 eneo la Kimara wilaya ya Ubungo, washtakiwa wanadaiwa kumuua kwa kukusudia, bondi wa ngumi, Thomas Mashali.

Mashali anadaiwa kufariki dunia kwa kushambuliwa na watu baada ya kusingiziwa ni mwizi na watu ambao aligombana nao, eneo hilo la Kimara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad