Waziri wa Maji Jumaa Aweso "Msoto Niliyopitia ni Kama Nabi wa Yanga"


Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameufananisha mtikisiko ambao ameupata kama Waziri wa Maji kutokana na changamoto za uhaba wa maji hususani katika Mikoa ya Pwani ikiwemo Dar es salaam na mtikisiko alioupitia Kocha wa Yanga wa Nabi.

Aweso amesema hayo leo mbele ya Rais Samia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Maji Kigamboni, Ugawaji wa Mitambo ya Kuchimba Visima na Mabwawa na Makabidhiano ya Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kidunda Kisarawe II - Kigamboni.

“Nawashukuru Wakuu wa Mikoa na Wilaya wote pamoja na Kamati zao za Ulinzi na Usalama, tulipitia mtikisiko, hali ambayo nilipitia Mimi Waziri wa Maji nataka nifananishe na hali aliyopitia Kocha wa Yanga, Nabi maana Timu kila siku inafanya vizuri lakini ilivyotokea mtikisiko wakamwandikia atabaki hukohuko Tunisia lakini Mungu si Athumani leo umepiga golo Mh. Rais Samia Suluhu Hassan umepindua meza hapa Kigamboni“

“Wizara yetu imepitia mtikisiko Watu wanatafuta nani Mzembe lakini Mhe Rais umekuwa pamoja na sisi umetupa moyo sana, nawashukuru Wana habari kipindi hiki cha mpito wangeweza kutumia kalamu zao vibaya lakini wametumia kalamu zao kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad