Wengi wa waliofariki katika ajali ya ndege ya Precision Air ni wale waliokuwa siti za mbele na kati ambao hawakuweza kufungua mikanda kwa haraka. Kuharibika sehemu ya chini ya ndege kuliruhusu maji mengi kuingia ndani kwa msukumo mkubwa, na kuwafunika.