Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or amekuwa mchezaji wa kutegemewa sana United tangu Ten Hag alipopokezwa mikoba ya kuinoa mnamo Mei 2022.
Ronaldo aliadhibiwa baada ya kukataa kuingia kama mchezaji wa akiba katika mechi dhidi ya Tottenham mnamo Oktoba ambapo United ilitwaa ushindi wa 2-0.
Hata hivyo, alirejea kikosini wiki jana na hata kukabidhiwa majukumu ya kuwa nahodha wa Mashetani Wekundu katika mechi waliyochapwa 3-1 na Aston Villa.
Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37, hakuwepo tena kwenye kikosi kilichosajili ushindi wa 2-1 dhidi ya Fulham siku ya Jumapili, Novemba 13 katika mechi ya mwisho ya United kabla ya mapumziko ya wiki sita ili kupisha mchuano wa Kombe la Dunia.
Akiwa katika mahojiano Jumapili, Novemba 13, na mahojiano na kipindi cha Televisheni cha Piers Morgan Uncensored, Ronaldo alisema haya kuhusu Ten Hag: "Sina heshima kwake kwa sababu haonyeshi heshima kwangu. Sio tu kocha, lakini vijana wengine wawili au watatu karibu na klabu. Nilihisi kusalitiwa."
Alipoulizwa tena iwapo viongozi wakuu wa klabu walikuwa wakijaribu kumfukuza, Ronaldo alijibu: "Ndiyo, nilihisi kusalitiwa na nilihisi kama baadhi ya watu hawanitaki hapa, si mwaka huu tu bali mwaka jana pia."
Awamu yake ya kwanza akiwa United ilikuwa ya mafanikio chini ya ukufunzi wa Alex Ferguson, akishinda mataji matatu ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa na taji la kwanza la Ballon d'Or kama mchezaji bora zaidi duniani.
"Tangu Sir Alex alipoondoka, sikuona mabadiliko katika klabu. Hakuna kilichobadilika," Naitakia mema klabu. Hii ndiyo sababu nimekuja Manchester United."
"Lakini kuna baadhi ya mambo ndani ambayo hayatusaidii (sisi) kufikia kiwango cha juu kama (Manchester) City, Liverpool na hata sasa Arsenal.. .klabu iliyo na mwelekeo huu inapaswa kuwa juu ya mti na kwa maoni yangu hawapo kwa bahati mbaya," Ronaldo aliongeza akizungumzia kuhusu kile alichokipata aliporejea United.
Licha ya mabao yake 24 katika michuano yote msimu uliopita, United walivumilia kampeni mbaya huku wakimaliza katika nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu ya Uingereza na kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.
United kwa sasa wako katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, wakiwa na pointi 11 nyuma ya vinara Arsenal.