Yanga Wanywe Kahawa ya Moto – Ushauri wa Rage


Wakati Yanga SC inajiandaa kushuka uwanjani kuwakabili Club Africain nchini Tunisia kesho Novemba 9, 2022 Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amewashauri Young Africans kunywa kahawa ya maziwa ya moto wakati wa mapumziko badala ya maji.


Rage ameyasema hayo kupitia Wasafi fm  ”Mara nyingi wenzetu wanapenda kucheza usiku, kunakuwa na ubaridi, niliwashauri Yanga ni kawaambia wahakikishe kwa Tunisia, wachezaji ndani wavae fulana zile nzito kidogo za mikono mirefu ambazo juu yake wanavaa jezi ili waweze kuwa ‘comfortable’.”


Rage ambaye amewahi pia kuwa kiongozi wa TFF kwa wakati huo ikiitwa FAT ameongeza  ”Na mapumziko badala ya kunywa maji wanatakiwa wanywe kahawa ya maziwa ya moto.”


”Niliwaambia wana Yanga wasikate tamaa kwasababu pia wanayofaida, timu ya Club Africain kwa vyovyote watafunguka. Sasa ule mchezo wa kupaki basi kama walivyofanya hapa hawatofanya. Nawasihi Watanzania wenzangu, Yanga inapocheza sio kwamba wanawakilisha wana jangwani au wananchi wanawakilisha watanzania.”


”Yanga wanachotakiwa kucheza ‘counter attack’, Sisi Simba SC tuliwashinda wale Watunisia kupitia Okwi, tulifanya dakika za mwisho ‘counter attack’ ikatusaidia tukapata goli moja na tukafuzu ndiyo ikawa mara ya kwanza kwa Tanzania kushinda Tunisia.


Yanga SC watawakabili Club Africain nchini Tunisi  majiri ya saa 2: 00 usiku kwa Tanzania ukiwa ni mchezo wa marudiano Kombe la Shirikisho Barani Afrika wakati mechi ya kwanza iliyopigwa Benjamin Mkapa dakika 90 zilimalizika kwa sare tasa ya bila kufungana.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad