Abiria wahofia kuzidishiwa nauli kwa Maguful




Abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali kupitia kituo cha mabasi cha Magufuli Dar es Salaam, wameitaka serikali kupitia LATRA kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa abiria juu ya ukataji tiketi mtandao kwa kuwa baadhi ya mabasi hayakatishi tiketi hizo na kuongeza nauli kwa abiria.
Wakizungumza na EATV leo Desemba 12, 2022, abiria hao wamesema kuna changamoto ya wananchi wengi hasa wale wanaosafiri kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kutofikiwa na elimu hiyo jambo linalosababisha kuendelea kukataa tiketi za mkono ambazo hazina bei za nauli elekezi kama zile za kieletroniki

Kwa upande wake Afisa Leseni Mfawidhi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) Eyudi Nziku, amesema serikali ilishapiga marufuku tiketi za mkono na imekuwa ikitoa elimu ya mara kwa mara kwa wananchi na kusisitiza kwamba abiria wote wanaosafiri kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kuhakikisha wanakata tiketi mtandao Ili kuepuka kuongezewa nauli.

Naye Meneja wa kituo cha mabasi cha Magufuli Isihaka Waziri, ameeleza ni kwa jinsi  gani kituo hicho kilivyojipanga kukabiliana na wimbi la idadi kubwa ya abiria wanaosafiri kuelekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka, huku akiwasihi abiria kuwa waangalifu na wapiga debe kwa kuwa kila basi lina ofisi zake ndani ya kituo hicho.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad