Argentina Yaingia Robo Fainali Ya Kombe La Dunia Qatar

 


Lionel Messi akishangilia ushindi wa 2-1 dhidi ya Australia katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia, Jumamosi, Desemba 3, 2022, mjini Rayyan, Qatar.

Argentina imekata tiketi ya kuingiabrobo fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuifunga Australia bao 2-1 katika uwanja wa Ahmed bin Ali Doha Qatar siku ya Jumamosi.


Lionel Messi aliyefungua mlango wa Australia katika dakika ya 35 ya mchezo. Na Julian Alvarez alipachika bao la pili katika dakika ya 57.


Vijana wa Australia hawakuonyesha kukata tamaa waliendelea kujibu mashambulizi kwa vipindi na hatimaye kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi katika dakika ya 77 baada ya mkwaju uliopigwa na Craig Goodwin na kumgonga mlinzi wa Argentina Enzo Fernandez na kuelekea nyavuni.


Argentina waliendelea kushambulia na kunako dakika za mwisho Lionel Messi alikosa nafasi ya wazi baada ya kupiga mkwaju aliokunja uende kwenye kona ya goli lakini ukatoka nje.


Hali kadhalilka ngome ya Australia ilifanya kazi kubwa kupambana na washambuliaji wa Argentina na kuokoa hatari nyingi chini ya golikipa wao Mathew Ryan ambaye alifanya kazi ya ziada.


Mchezaji wa Australia mwenye asili ya Sudan Kusini almanusura afunge bao la kusawazisha mwishoni mwa kipindi cha pili katika dakika za majeruhi baada ya kupiga shuti akiwa katika nafasi nzuri yeye na golikipa lakini golikipa wa Argentina Emiliano Martinez alifanikiwa kuokoa hatari hiyo.


Hadi mwisho wa mchezo Argentina 2 Australia 1 na kuwa ndio mwisho wa safari ya Australia.


Kwa maana hiyo Argentina sasa itakumbana na Uholanzi kwenye robo fainali Ijumaa.


Vijana wa Australia -Spocceroos safari yao imeishia raundi ya pili lakini wameshangza ulimwengu wa soka kwa kuingia raundi ya 16 kwa kuwaangusha Denmark na kucheza kwa hali ya juu dhidi ya vigogo wa soka duniani Argentina.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad