Askari adaiwa kumuua mkewe kwa risasi



Afisa wa polisi anayehudumu katika kituo cha polisi cha Bamburi mjini Mombasa amekamatwa kufuatia kifo cha mkewe.

Emily Masinza aliaga dunia kutokana na majeraha alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Coast General. Picha: K24. Chanzo: UGC

Afisa huyo, Meshack Kosgey anadaiwa kumpiga risasi mkewe Emaily Masinza mwenye umri wa miaka 30 na kumuua kinyama.

Polisi waliripoti kuwa Kosgey alikuwa amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Nyali huku maaskari wakihangaika kukamilisha uchunguzi wao.


"Kwa sasa mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Nyali akisubiri polisi kukamilisha uchunguzi. Sasa atashtakiwa kwa mauaji ya marehemu kinyume na kifungu cha 203 cha kanuni ya adhabu," ripoti ya polisi ilisema.

Taarifa za awali zimeonyesha kuwa ndoa ya Kosgey ilikuwa na matatizo na alimpiga risasi baada ya kutishia kuvunja uhusiano huo.

Topister Juma, afisa wa jinsia huko Muhuri aliambia Citizen Digital kwamba wawili hao walikuwa na ndoa yenye matatizo.


Alisema wawili hao walikuwa wakizozana sana na hata baada ya kuhama kutoka kambi ya polisi waliendelea.

“Ilikuwa ni ndoa ya malumbano hata wakatoka wanaishi nje ya kambi...huko nje mambo ilikuwa ni hayo hayo," alisema.

Kulingana na babake, John Azangu, alikuwa amemwagiza bintiye kufunga virago vyake na kuacha ndoa ya miaka mitatu kabla ya kuarifiwa kwamba alikuwa amepigwa risasi.

“Mwezi Oktoba alisema amepigwa na akamnyang’anya kitambulisho chake. Nikamwelezea funga virago akufuate huku nyumbani ni Krismasi. Juzi napigiwa simu eti msichana amepigwa risasi,” alisema Azangu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad