Polisi wa eneo Bunge la Kandara, Kaunti ya Murang'a nchini Kenya wanamshikilia mume pamoja na mkewe wenye watoto wanne wa kike baada ya mtoto wao kufichua kuwa baba yao amekuwa akiwabaka.
Mume huyo anasemekana kufanya vitendo hivyo vya kuogofya huku mkewe akifahamu kikamilifu matendo yake nyumbani kwao Gichengo-Muruka.
Kulingana na ripoti, mkewe alinaswa baada ya mmoja wa binti zake wanne kukiri kuwa alipachikwa mimba na babaake huku mama yake akijua.
Wakazi walisema kwamba msichana wa miaka 14 ambaye alikuwa amemaliza darasa lake la nane alikuwa amepachikwa mimba pamoja na dadaake.
Walisema baba huyo alijaribu mara kwa mara kulala na binti zake wote wanne katika matukio tofauti na wengine wawili waliokolewa tu na majirani baada ya kupiga mayowe.