Balaa Ni Zito !! Kama Kutakuwa Na Ukweli Kwenye Kauli Za Baba Wa Rapa #ToryLanez "Sonstar Peterson" Kuhusu Uhusika Wa #Jayz Kwenye Sakata La Kupigwa Risasi Kwa Rapa #MeganTheeStallion Lililodaiwa Kufanywa Na Tory Lanez Huenda Suala Hili Likamuweka Kwenye Matatizo Jayz.
Mapema Leo Wakati Kesi Ya Tory Lanez Imefika Mwisho Na Kukutwa Na Hatia Ya Mashtaka Yote Matatu (3), Mzee Sonstar Peterson Alipiga Kelele Nje Ya Mahakama Huko Los Angeles Akimtuhumu Jayz Ambaye Ni Mwanzilishi Wa Kampuni Ya Roc Nation Ndio Amehusika Kwenye sakata Zima
Baba Yake Tory Anadai Kuwa Jayz Amehusika Asilimia 100% Kwenye Hili Kwasababu Tory Aligoma Kusaini Mkataba Chini Ya Roc Nation Lakini Pia Kuna Taarifa Zinadai Kwamba Megan Alighushi Kupigwa Risasi Kwa Madai Ilikuwa Ni Mbinu Ya Uuzaji Iliyobuniwa Na Rapa #Jayz.
(Jayz Alimsaini Megan Roc Nation 2019)
Sababu Nyingine Aliyoitaja Mzee Na Kuilamu Mahakama Ni Kwamba Uchunguzi ulibainisha kwamba Vinasaba (DNA) vya Tory Lanez havikuonekana kwenye silaha ambayo ilitumika Kumpiga Risasi Megan Julai 2020, Sasa Inakuaje Tory Atajwe Kama Mhusika Wa Tukio Hilo
"Mfumo Huu Wa Mahakama Sio Wa Haki Kabisa ...Na Wanafanya Machafu Kila Wawezavyo!!. JAYZ Ngoja Niongee Na Wewe ...! Ni Kwasababu Mwanangu Alikataa Kusaini Dili La Roc Nation Na Wewe"
"Jayz Na Beyonce Hata Nyie Mna Watoto Ngoja Tuone sasa ! Nyie Ndio Sababu Ya Wengine Kwenda Jela .....!! Beyonce Na Jayz Mimi Ni Mtumishi Wa Mungu Mtajua Mimi Ni Nani" - Baba Na Mama Wa Kambo Wa Tory Lanez
Kumbuka Tu Kuwa Tory Lanez Hukumu Yake Imepangwa Jan 27, 2023, Anakabiliwa na miaka 22+ Jela