Babu Tale "Sipendi Hata Kumuona Rayvanny Ameniumiza Sana"


Mbunge wa Morogoro kusini Mashariki na Meneja kutoka Record Label ya WCB, @babutale amedai kati ya vitu vinavyo muumiza kwenye maisha yake, kimojawapo ni kuondoka kwa @rayvanny WCB, Tale amedai anampenda sana #Rayvanny kiasi kwamba imekuwa ngumu kukubali kuwa msanii huyo hayupo tena Wasafi.


Amplifaya na Millardayo.com imefanya exclusive interview na Babu Tale ambapo amedai hataki hata kumuona Rayvanny, kusikiliza nyimbo zake hata wakati mwingine hapokei simu zake, si kuwa anamchukia, ila roho inamuuma anapoona hayupo karibu naye kama ilivyo kuwa awali, hivyo kuona vitu vyake hata simu zake ni kutonesha jeraha lenye uwingi wa maumivu ya Rayvanny kuondoka WCB.


Tale pia amedai bado pesa kidogo zimesalia kwa Rayvanny kuilipa WCB ili kuachana kabisa na Label hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad