Baiskeli Chanzo Kifo Cha Mwandishi wa TBC Mlima Kilimanjaro


Mwandishi wa Habari na mpiga picha wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Joachim Kapembe (45) amefariki dunia kwa ajali ya baiskeli wakati akishuka kutoka Mlima Kilimanjaro.

Mwandishi huyo pamoja na wenzake walipanda Mlima Kilimanjaro, Desemba 9 mwaka huu kwa ajili ya uzinduzi wa mawasiliano ya intaneti kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 14 na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Catherine Mbena inasema kuwa Kapembe alifariki Desemba 13 saa 12:00 jioni katika Kituo cha Kibo Hurt kutokana na ajali ya baiskeli aliyokuwa akiindesha kama sehemu ya utalii.

"Kapembe katika uhai wake alikuwa mtumishi wa TBC na alikuwa mmoja kati ya watu ambao walipanda Mlima Kilimanjaro wakati wa kwenda kuzindua mtandao wa intaneti katika kilele cha uhuru," ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, Kapembe alifikwa na umauti wakati waa kushuka kutoka kilele cha Uhuru baada ya kupata ajali ya baiskeli aliyokuwa akiendesha kutoka kituo cha Kibo kuelekea kituo cha Horombo.

"TANAPA inatoa pole kwa familia ya marehemu , watumishi wa TBC, Wanahabari na Taifa kwa ujumla kwa kupoteza nguvu kazi ya Taifa,"

Mawili wa Mwandishi huyo umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini, KCMC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad