Basata Wausifia WIMBO wa Dula Makabila, Wasisitiza Usikilizwe

 


Katibu Mtendaji wa BASATA, Dr Kedmon Mapana amesifia sana Wimbo huu, kwani Dulla ameumiza sana kichwa kutunga na kuibuka na Mistari Bora kabisa, zaidi amesisitiza kwamba Watu wasikilize wimbo mzima wasisikilize kipande tu, hasa kile cha Aggrey.


Mapana amesisitiza wasanii wasipaone BASATA kama kituo cha polisi bali ni kwa walezi wa sanaa, hivyo wasanii wasiogope kabisa wakiitwa mahali hapo.


Makabila amesema baada ya kupokea ujumbe kuwa anaitwa na BASATA akili iliyumba kidogo, akajua kifuatacho ni kufungiwa kwa nyimbo yake lakini alipoenda hali ilikuwa tofauti


Makabila amefunguka kwamba hii ndio ngoma yake ambayo ametumia Hela nyingi sana kuindaa, lakini hajutii hilo maana imepokelea vizuri kuliko ngoma zake za awali.


Kubwa zaidi Dr Mapana amesema Dhumuni la Kumuita Dula na Vyombo vya habari ni kusisitiza Watu wasikilize wimbo mzima, wasisikilize tu kile kipande kinacho-trend mitandaoni, maana wakisikiliza pale tu watahisi wimbo huu unapotosha Jamii.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad